kongamano la nane mjini Eldoret

Maandalizi ya kongamano la ugatuzi linaloanza mjini Eldoret wiki hii yamekamilika kuanzia Agosti 15-19 huku Rais William Ruto, Naibu wake Rigathi Gachagua na kinara wa upinzani Raila Odinga wakitarajiwa kuhudhuria.

Wajumbe wameanza kuwasili kabla ya kongamano hilo linalofanyika kila baada ya miaka miwili, ambalo litaanza Jumanne na kumalizika Ijumaa.

Rais Ruto atafungua rasmi Mkutano huo Jumatano, na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair atakuwa miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Ratiba iliyotolewa na Baraza la Magavana CoG inaonyesha kuwa Odinga atahudhuria hafla hiyo Alhamisi, huku naibu rais Gachagua akilifunga rasmi Ijumaa.

Zaidi ya wajumbe 10,000 wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria.

Kulingana na Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii,amesema  maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika, ingawa wazazi na wanafunzi wa Mpango wa Elimu ya Ng’ambo katika kaunti ya Uasin Gishu wametishia kufanya maandamano kila siku wakati wa kongamano hilo wakitaka warejeshewe pesa zao.

Wazazi hao wamekuwa wakifanya maandamano mjini Eldoret wakitaka kurejeshewa pesa zao baada ya watoto wao kukosa kusafiri kuenda ng’ambo kwa masomo zaidi licha ya kulipa mamilioni ya pesa kwa serikali ya Jackson Mandago.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *