hakuna ubaguzi kwa masomo

Naibu rais Rigathi Gachagua ameweka bayana kwamba mabadiliko kwenye sekta ya elimu ni kwa manufaa ya wakenya wa tabaka zote nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya 41 ya kufuzu kwa mahafali katika chuo cha Eastren Africa Baraton katika kaunti ya Nandi Gachagua amesema kwamba serikali inalenga kuwasaidia wakenya wote bila ya miegemeo yoyote ya maisha akijitenga na uvumi kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuwatenga watoto kutoka familia maskini.

Ameyazungumzia haya baada ya serikali kupitia idara ya Elimu kufanya mageuzi kwenye ufadhili wa masomo kwa wanafunzi walio kwenye vyuo vikuu ,vya kadri na vya kuifundi kuwapa ufadhili wanafunzi kutoka familia maskini.

Naibu huyo kadhalika amewataka wanafunzi kujituma shuleni na kuhakikisha wanafuata kwa ukamilifu ndoto zao na hili akiwaeleza kwamba wataafikia ndoto hizo bila ya vikwazo vyovyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *