Naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Mhandisi John Barorot amesema kwamba hatua za kisheria zitachuguliwa dhidi ya watu na viongozi watakaopatikana kuhusika kwenye sakata ya ,masomo ya mataifa za ufini na Canada ambao umezua tumbojoto miongoni mwa waliokuwa na wakuu wengine katika serikali ya kaunti ya Uasin Gishu.
Akizungumza katika hafla ya mchango wa ukamilisho wa ukumbi wa kanisa la Moyo mtakatifu wa Yesu Kathedrali hapa mjini Eldoret,Barorort amesema kwamba tayari wanafunzi zaidi ya arobaini wanatarajiwa kusafiri Finland juma lijalo kuendeleza masomo yao huku uchunguzi ukiwa unaendelea.
Wakati huo naibu huyo ameweka wazi kwamba serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imeweka mpango wa kubuni mbinu za kuwafikia viongozi wa kaunti kwa njia mwafaka ili kupunguza tofauti zinazotakana na matakwa yao kukosa kutatuliwa na kuimarisha uhusiano baina ya serikali na wakaazi.