Jitengeni na ubinafsi

wakristu wamehimizwa kuwa waaminifu kwa kristu na kujitenga na mambo ambayo huenda yakawaweka mbali na mwenyezi mungu.

Akiongea katika kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali padre Peter Paul Idiama alisisitiza kwamba ukristu unahitaji mwekeleo bora na kwa huyo mkristu kujisadaka bila kujibakisha kwa kujenga imani yake dhabiti katika kristu ambaye atawaongoza kwa njia iliyosalama.

Padre alisema kwamba ili mkristu aweze kudhihirisha ukristu wake kwa wengine na kuwa mfano mwema kwao,anapaswa kujitenga na ubinafsi maana litamsongesha mbali na mwenyezi mungu.

Alidokeza kwamba japo changamoto ni nyingi kwa mwanadamu wanapaswa kutokata tamaa maishani mwao ila wamtangulize kristu ambaye atawasaidia kukua kiimani na kuuridhi ufalmwe wa mbingu.

Kadhalika,aliwashauri wakristu kutokubali kuongozwa na tamaa akieleza inachangia pakubwa kudorora kwa imani yao kwa kristu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *