Halalisheni ndoa yenu kanisani

Wito umetolewa kwa wanandoa kuhalalisha ndoa yao kanisani ndipo iweze kufungua njia ya kutimiza mahitaji yao katika jamii na kanisani.

Kulingana na askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo ni kwamba ni kupitia familia hizo ambapo kanisa itaongeza idadi ya watumishi katika shamba la bwana na hili kuwasaidia wanajamii kujenga imani katika kristu.

Alisisitiza kwamba wito wa ndoa imebarikiwa na wanastahili kutohofu lolote maana mwenyezi mungu atawaongoza kila muda wakiwa katika maisha hayo.

Vilevile,Askofu Anyolo aliwataka watoto kuwa na heshima kwa wakubwa na pia wadogo wao kwa kuwasikiza wazazi wao kwa mawaidha wanayopewa ndipo wawe na maisha yenye baraka akieleza kwamba heshima kwa wakubwa na wadogo ni baraka kutoka mwenyezi mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *