Mzozo kuhusu ufadhili wa masomo kaunti ya Uasin Gishu kwenda mataifa ya Ufini na Canada unaendelea kutokota huku wazazi wakiapa kurejea makwao iwapo watapewa pesa zao na serikali ya kaunti hiyo.
Wakizungumza nje ya makao makuu ya kaunti mjini Eldoret, wazazi wa wanafunzi hao wamesema wataendelea kukita kambi nje ya malango ya kaunti hadi watakapo rejesheshwa pesa zao zikiwa pesa taslimu.
Walisema hawana haja tena na ufadhili wa masomo hayo ambayo kwa wnegi wanao wamesalia nchini kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kulipa pesa kwa lengo la wanao kusafiri katika mataifa za Ufini na Canada,sasa wanasema warudishiwe pesa hizo mara moja kwani wameweka bayana kwamba hawahitaji tena wanao kusafiri.
Yanajiri haya huku gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim na seneta Jackson Mandago wakitarajiwa kuzungumza na waathiriwa hao baada ya kuandaa mkutano waadhara.