Kapu la taifa litaongezwa kwa uwepo wa mikakati

Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Uasin Gishu wanaitaka serikali kuweka mikakati ya kuteremsha bei ya pembejeo zingine za ukulima kando na mbolea ili gharama ya uzalishaji iweze kurudi chini.

Wakulima hawa wanasema kwamba japo wamefurahia mpango wa serikali wa kuteremsha chini bei ya mbolea itakua sawa pia iteremshe bei ya mafuta wakisema kwamba mafuta pia ambayo kwa wakati huu yamepanda sana yanachangia kupanda kwa gharama ya uzalishaji.


Wakuzungumza MjiniĀ  Eldoret wakulima hao pia walilalamikia kupanda kwa bei ya mashine ambazo wanatumia kwenye ukulima jambo ambalo pia wanaitaka serikali kuliangazia .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *