wazee wa mtaa wafaidika na tonge la kila mwezi

Kufuatia hatua ambayo serikali imechukua kuwatunuku shillingi eflu Saba Kwa wazee wa mtaa Kila mwezi kama mshahara wao,baadhi ya wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu wamepongeza mpango hao  wakisema itasaidia kuwawezesha kutia bidii kazini na pia maisha yao yataweza kubadilika.

Wakizungumza mjini Eldoret walisema kwamba wazee wa mitaa wanafanya kazi mingi hasa ya kutatua mizozo na kwa muda mrefu wamekua wamesahaulika na itakua bora iwapo serikali imezingatia wazo hilo ambalo miaka zinaposonga serikali itawaongezea mishahara hata  zaidi.

Hata hivyo walipendekeza wanakijiji waruhusiwe kuwachagua wazee wa mitaa ambao wanawataka wakisema kwamba wao ndio wanafahamu zaidi wazee ambao wanaishi nao na ambao wataweza kutekeleza kazi hiyo kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *