Maridhiano yasiyoegemea upande wowote

Viongozi wanoegemea mrengo wa upinzani katika magharibi mwa nchi walitaka kuwepo kwa maridhiano baina ya rais William Ruto na Kinara wa Azimio Raila Odinga kwa njia ya uwazi bila ya kushurutishwa.

Wakiongozwa na gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa na naibu wake Ayub Savula waliwataka wawili hao kuandaa mazungumzo ya haraka ili kuokoa taifa kutokana na gharama ya juu ya maisha ,mazungumzo ambayo wanasema hayapaswi kuegemea upande wowote bali ni kwa manufa aya wakenya.

Viongozi hao vilevile wamewataka viongozi ambao wana nia ya kutoruhusu maongezi hayo kukaa mbali na hatua hiyo kwani wanaeleza kwamba wakenya wameumia kwa muda sasa na iwapo viongozi hao wanasema ni wabinafsi wataingilia kati huenda itazamisha uwepo wamaafikiano na hili wamesema halistahili hata kidogo.

Haya yanajiri huku muungano wa azimio la umoja one Kenya ukizindua mpango wa kuchangisha fedha ili kufanikisha mazishi ya watu waliouawa wakati wa maandamano dhidi ya serikali.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba ya vigogo wa Azimio, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amedokeza kwamba kinara wa muungano huo Raila Odinga na rais mstaafu Uhuru Kenyatta tayari wametoa shilingi milioni moja kila moja kufanikisha  mazishi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *