wote yapata jimbo jipya

Baba mtakatifu Francisko amebuni jimbo katoliki jipya la Wote na kumtangaza Askofu Paul Kariuki Njiru kama mwanzilishi wa jimbo hilo.

Kwenye taarifa iliyochapishwa katika waraka rasmi kule Roma saa saba mchana majira ya afrika mashariki na kutangazwa na mwakilishi wa baba mtakatifu nchini na Sudan Kusini mwadhama Mathews Hurbetus Maria Van Megen, jimbo hilo katoliki la wote limebuniwa kutoka katika jimbo katoliki la Machakos Askofu Paul Kariuki akiteuliwa kuwa mwanzilishi wa jimbo hilo.

Hadi kuteuliwa kwake Askofu Paul kariuki amekuwa mchungaji wa jimbo katoliki la Embu.

Askofu paul kariuki alizaliwa tarehe 11 mwezi Marchi 1963 kule Githunguri Kyeni chini ya jimbo katoliki la Meru kisha baadaye aksomea somo la falsafa katika seminary ya Meru kati ya mwaka wa 1985-1987, na kisha baadaye akasomea somo la tiolojia katika seminari kuu ya mtakatifu Toma wa Akwino Langata kati ya mwaka wa 1988-1991.

Baada ya masomo na majiundo na kadhalika kuhudumu katika parokia mbalimbali katika jimbo katoliki la Meru akateuliwa kuwa Askofu wa jimbo katoliki la Embu tarehr 9 mwezi May 2009 na baba mtakatifu benedikto kwa kumi na sita.

Kubuniwa kwa jimbo hili la Wote sasa inafikisha idadi jumla ya majimbo katoliki nchini kuwa ishirini na tano ikijumuisha jimbo la wanajeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *