Shinikizo zaidi zinazidi kutolewa kwa rais William Ruto na kinara wa muungano wa upinzani Raila Odinga kuweka kando misimamo mikali, na kuipa kipaumbele mazungumzo kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza baada ya kuadhimisha misa ya vikundi mbalimbali vya sala chini ya jimbo hili katoliki la Eldoret, Askofu Kimengich ametoa wito kwa viongozi hao wakuu kuketi pamoja na kujadiliana kuhusu maswala tata, yakiwemo hali ya juu ya gharama ya maisha miongoni mwa maswala mengine yanayowasakama Wakenya kwa sasa.
Askofu kadhalika amewataka maafisa wa polisi kukoma kutumia nguvu kupita kiasi, wanapokabiliana na waandamanaji akisema kuwa wanaovunja sheria kwa kuandamana wanastahili kukamatwa na kushtakiwa mahakamani.