KCCB yahimiza maridhiano

Baraza la maaskofu wa katoliki nchini KCCB unapendekeza uwepo wa mazungumzo kati ya viongozi wakuu nchini Rais William Ruto na Kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga ili suluhu na mwafaka kuafikiwa kufuatia maandamano yanayooongozwa na Upinzani ya kushinikiza serikali kupunguza gharama ya maisha.

Baraza hilo likongozwa na mwenyekiti wake ambaye pia ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva ni kwamba viongozi wa kidini wako tayari kusaidia katika upatikanaji wa suluhu la kudumu wakieleza kwamba kuna njia mbadala ya kutatua changamoto ,malilio na mahitaji ya wakenya kwa njia iliyo salama na sio ya kuandamana kwa kuharibu usalama na maendeleo ya nchi.

Vilevile viongozi hao waliongeza kwamba mazungumzo hayo yatachangia pakubwa ukuwaji wa taifa hili na amani iweze kuendelea kuwepo.

Wakati huo,viongozi hao wamewashauri wakenya kuendelea kuwa na subra licha ya changamoto zinazoshuhudiwa kwa sasa wakidokeza kwamba pandashuka za maisha zinazowakabili wakenya kwa sasa zinaweza zikatatuliwa kwa uwepo wa maridhiano na wakenya kuweza kukumbatia amani kila wakati,na kuongeza kwamba zipo njia nyingi za kutatua uhasama na sio tu kwa kuharibu maendeleo ya nchi.

Aidha,kccb imekashifu jinsi ambavyo maafisa wa usalama wanatumia nguvu kupita kuwkabili waandamaniji ikisema kuwa polisi wanastahili kuwapa waandamanaji usalama badala kukabiliana nao.

Yanajiri haya wakati na ambapo upinzani ikiongozwa na Kinara wake Raila Odinga ukiapa kuendeleza maandamano ya siku tatu kwa wiki kuanzia siku ya jumatano hadi ijumaa kushinikiza serikali kuangazia kupunguzwa kwa gharama ya maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *