kaunti ya Uasin Gishu ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano la kumi na moja la ugatuzi ifikiapo mwezi wa Agosti mwaka huu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amesema kuwa kongamano hilo litakuwa la manufaa kwa kaunti hii kiuchumi.
Katika kikao na wanahabari hii leo afisini mwake alipowapokea kamati tendaji ya ugatuzi, gavana Jonathan Bii amesema kuwa maandalizi ya kuandaa kongamano hilo yameshika kasi yakiwemo ukarabati ya barabara zote katika kaunti hii usafi wa mazingira na kuweka taa katika barabara zote.
Gavana bii kadhalika amewakikishia wale watakaohudhuria kongamano hilo usalama wao, akisema kuwa maafisa wa usalama tayari wameweka mikakati kabambe katika siku hizo za kongamano, akitoa wito kwa wenyeji kuchukua fursa hiyo kutangamana kwa faida ya ukuaji wa kaunti hii.
Naye mwenyekiti wa kamati tendaji ya ugatuzi ambaye pia nia gavana wa Wajir Mohamed Abdulahi amesema kuwa kongamano hilo linanuia kupiga jeki ukuaji wa serikali za gatuzi nchini