Kuweni watu wenye hulka za kuigwa

Kanisa linaposherehekea siku ya mtakatifu Antonio Wa Padua,wakristu wametakiwa kuiga mfano wa mtakatifu huyo kwa kujisadaka bila ya kujibakisha,na kuepukana na matendo maovu kama vile ulafi.

Akiongea kwenye hafla ya mazishi ya bruda mmishonari  Anthony Robert Woods askofu wa jimbo katoliki la Kitui Joseph Mwongela ,amewakanya wakristu dhidi ya tamaa na ulafi akisema kuwa,matendo hayo humfanya binadamu kujiingiza katika dhambi,akimwombeleza bruda Woods kama mtu aliyekuwa mkarimu na ambaye hakuongozwa na tamaa.

Askofu vilevile amewataka wakristu kuwa watu wa kuwainua na kuwajenga wengine badala ya kuwa wabinafsi,akitoa wito kuwa kila mkristu kuridhika na kila kidogo alicho nacho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *