Tutajisimia wenyewe

Muungano  wa makanisa ,wahubiri na makasisi katika kaunti ya Uasin Gishu waliwataka viongozi wa kisiasa kutoingiza swala la madhehebu siasa wakisema kwamba wanayumbisha imani wa waumini.

Wakiongozwa na mwenyekiti wake askofu Hadson Ndeda lilisema kwamba makanisa yapewe jukumu la kujisimamia ndipo wahubiri potofu wapate kutambuliwa mapema.

Wakiongea mjini Eldoret,viongozi wa muungano huo walisikitikia namna wanasiasa wametumia swala utovu wa kinidhamu kutoka kwa baadhi ya wahubiri kuwachafulia mwonekano viongozi wengine wa kidini wakisema sharti swala hilo likomeshwe mara moja.

Sasa walipendekeza kwa serikali ya kitaifa viongozi wa madhehebu hayo kupewa nafasi ya kuandaa kikao na kujadili namna wanaweza wakapambana na wanaojaribu kuharibu sifa na kuwaelekeza waumini kwenye njia isiyokuwa sawa.

Yamejiri haya huku jopo maalum lililotwikwa jukumu la kutafuata maoni kutoka kwa viongozi wa kidini na namna ya kurejesha hadhi ya madhehebu na maeneo ya kuabudu iweze kurejeshwa ukiwa mbioni kukamilisha jukumu lake hii ni baada ya kisa cha kusikitisha cha mhubiri tata Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International kuwaadaa washiriki wake kujinyima kula hadi kufa ili kukutana na mwenyezi mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *