wakenya waendelea kukaza kamba

Ipo haja ya serikali kuangazia upya pendekezo la kuwatoza ushuru wakenya, pendekezo ambalo huenda likamkandamiza mkenya, na badala yake kuweka mikakati zaidi itakayoangazia maisha ya mkenya wa tabaka la chini.

Askofu wa Jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich alisema kuwa ingawa serikali ina haki ya kuweka mikakati ya kukusanya ushuru ambayo itasaidia katika ukadiriaji ya miradi mbalimbali ya maendelo nchini, serikali hiyo kadhalika ina jukuma la kuhakikisha kuwa mikakati hiyo inawekwa kwa faida ya mkenya wa tabaka la chini wala sio kumnyanyasa.

Alitoa wito kwa wakenya kuvumilia hali ya sasa ambayo yanashuhudiwa nchini kiuchumi kwa kuipa serikali muda wa kuangazia jinsi itakavyokwamua wakenya kutoka na hali hiyo mgumu wa kiuchumi.

Hata hivyo askofu Kimengich alitoa wito kwa wale walio kwenye mrengo wa upinzani kushirikiana na serikali kwa njia ya mazungumzo ili kupata suluhu la changamoto ambayo kwa sasa imewasakama wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *