Wakuu katika shule mbalimbali na walimu wa shule za humu nchini walitakiwa kuwa mstari wa mbele kuwaelekeza wanafunzi katika njia salama na za heshima wakiwa shuleni kuepuka utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi hao.
Akiongea kwenye hafla ya kila mwaka ya shule zinazodhaminiwa na jimbo katoliki la Eldoret,padre mkuu wa jimbo la Eldoret William Kosgey alisema kwamba iwapo jamii inalenga kuhitimisha maswala ibuka na ambazo hazistahili katika jamii,yawapasa walimu kuwasaidia vijana kupambana na hulka ibuka ambazo zinawaelekeza kwenye vikundi potofu swala analosema sharti wapewe mawaidha ndipo waweze kujitenga nazo.
Padre mkuu vilevile aliwataka washidakadau mbalimbali kwenye sekta ya elimu kwenye shule zinazofadhiliwa na jimbo la Eldoret kuhakikisha kwamba wanawasaidia wanafunzi kuweka hadhi ya juu ya nidhamu ambayo kila mmoja anaweza kuitamani kuiga kwa kuwapa mwelekeo ulibora katika maisha akisema kwamba uongozi wa kesho imo mikononi mwa wanafunzi hao.
Aliwahimiza wanafunzi hao kukua na uhusiano mwema kwa kuungana mikono kama wanafunzi ndipo waweze kutimiza ndoto zao za masomo na kuweza kuafikia malengo ya maisha yao huku akiwataka kujitenga na tofauti baina yao inayochochewa na ushindani mbaya wanapopambana masomoni.