Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Uasin gishu Khalif Isaack Hassan alipuzilia mbali ripoti iliyochapishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini kuwa shule ya msingi ya Muget eneobunge la Moiben kaunti ya Uasin gishu imefungwa kufuatia ukosefu wa walimu shuleni humo.
Akiongea na wanahabari hapa mjini mkurugenzi huyo alipuuzilia mbali ripoti iliyodai kuwa shulee hiyo imefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia ukosefu wa walimu mtaala mpya wa umilisi cbc katika ngazi ya sekondari ya kiwango cha chini JSS, akisema kuwa shule hiyo ina walimu wakutosha na waliohitimu ambao kulingana naye hadi kufikia sasa wanaendelea na huduma yao katika shule hiyo, akisema kuwa madai ya baadhi walioandamana siku jumatatu wakidai shule hiyo haina walimu hayana msingi.
Khalifa alikariri kuwa walimu wanaofanya kazi katika shule hiyo wote walipata mafunzo katika ngazi mbali mbali yakiwemo ya kuwahudumia wanafunzi wanaotumia mtaala mpya wa umilisi CBC.
Alisema kuwa shule ya wavulana ya Kipsangui iliyofungwa muhula uliopita kufuatia mzozo baina ya wanakijiji na usimamizi wa shule hiuo imefunguliwa tena baada ya utata huo kutatuliwa, mwalimu mkuu wa shule hiyo akihamishwa na mwengine mpya kupewa jukumu la kusimamia shule hiyo.