SERIKALI YASTAHILI KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO

Wakulima katika kaunti ya Uasin Gishu wameiomba wizara ya kilimo nchini kuweka mikakati ya kutosha kwa wakulima kupata pembejeo kwa wakati ufaao kama njia moja ya kupunguza gharama ya uzalishaji.

Wakiongozwa na mzee Kolum wakulima hao walisema kwamba iwapo serikali kupitia wizara kilimo haiwezi kugharamia bidhaa zote za kilimo, ibuni mbinu ya kuwalipisha wakulima kwa njia mkopo ndipo wakulima wengi waweze kuendeleza vyema kilimo chao kila msimu wa upanzi unapowadia.

Wakulima hao vilevile walisema kwamba wanategemea sana kilimo katika kujikimu kimaisha na yapasa wizara hiyo kuwa makini kwa mipangilio yake isije ikayumbisha sekta na wanaotegemea kitengo cha ukulima.

Aidha,wakulima hao walisisitiza haja ya kupunguzwa kwa bei ya mafuta aina ya diseli ndipo ukulima uzidi kuinuka na wakenya wengi waweze kupata lishe bora kupitia ukulima nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *