Wagonjwa wa matatizo ya kiakili ( bipolar) wanaitaka serikali kuweka mikakati ifaayo ili kupunguza matibabu ya ugonjwa huo ambayo wanasema iko juu mno.
Wakizungumza mjini Eldoret wakiongozwa na Winnie Omondi walisema kwamba bei ya madawa wanayotumia ni ghali mno baadhi yao wakisema wanashindwa kuyanunua na kwamba bima ya afya ya NHIFÂ haiwezi kuwasimamia kununua madawa hayo jambo ambalo wanaitaka serikali kuingilia kati na kutatua swala hilo.
Wakati huo,wataalamu wa ugonjwa huo katika kaunti ya Uasin Gishu wanazitaka serikali za kaunti kuweka mikakati ya kuhakikisha hospitali za kaunti zinaweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa matatizo ya akili karibu na maeneo wanayotoka.