Tunaaswa kupewa nafasi za kazi kwa kujitolea kwetu

Viongozi waliosimamia uchaguzi mkuu uliopita wa Agosti tisa mwaka jana kupitia chama cha United Democratic alliance UDA katika kaunti ya Uasin Gishu walisema kwamba serikali iliwasahau baada ya uchaguzi huo na sasa wanadai nafasi za ajira kwa utendakazi wao.

Viongozi hao wanasema kwamba katika shughuli nzima ya kuwasajili wanachama hata kabla ya uchaguzi wallihakikisha wamefanikisha zoezi hilo na kumhakikishia rais William Ruto anapata kura nyingi za kumwezesha kuwa rais.

Wakiongozwa na Sammy Busienei wakizungumza nje ya afisi za UDA viungani mwa mji wa Eldoret,viongozi hao walisema kwamba wanaimani watapata nafasi za kazi baada ya kujituma kumwezesha rais Ruto kuingia madarakani.

Aidha ,viongozi hao walibaini kwamba wanaamini walifanya kazi yao kwa uangalifu na wanaeleza wanastahili pia wao kutuzwa kwa bidii yao.

Ikumbukwe kuwa kaunti ya Uasin Gishu ina wadi 30 na kila wadi ilikua na mratibu wa chama hicho cha UDA wakati wa uchaguzi ambapo viongozi hao wanadai nafasi za kazi serikalini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *