Wanafunzi 264 katika kaunti ya Elgeyo Marakwet watanufaika na ufadhili wa masomo ya shillingi millioni 2.5 kutoka ofisi ya mwakilishi wa kike kaunti hiyo.
Akiongea wakati wa kuzindua zoezi hilo,mwakilishi wa kina mama Caroline Ngelechei alisema ufadhili huo unalenga kuwafaidi wanafunzi kutoka familia zisizojiweza ,huku akiwapa chakula wahanaga wa njaa hasa walioathirika na uvamizi unaoendelea wa wizi wa mifugo Kerio Valley klwa kuwapa chakula gunia 300 ya Michele,gunia 250 ya maharagwe na gunia 200 ya mahindiĀ .
Hata hivyo Ngelechei alidokeza kuwa anapania kuanzisha kituo Cha uokozi cha kina mama na wasichana wanaopitia dhuluma katika kaunti hiyo.