Familia Moja ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 37 anayedaiwa kuaga wakati wa kujifungua katika hospitali ya mafunzo na Rufaa ya Moi Eldoret inalilia haki Kwa mpendwa wao Kwa kile wanasema utepetevu kutoka Kwa madaktari.
Familia hiyo ikiongozwa na nduguye marehemu Bernard Gitonga inasema kwamba marehemu Loice Njoki alifariki muda mfupi baada ya kujifungua mtoto Kwa njia ya upasuaji ,na licha ya upasuaji huo familia inadai haikupewa faili ya mgonjwa huyo kwa wakati ili kuwezesha madaktari waliofanya upasuaji huo kubaini kiini haliso Cha kilichopeleka kifo Cha Njoki.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa hospitali ya MTRH Dkt.Wilson Arwasa alikana madai hayo Kwa anachosema Njoki alishughulikiwa na wataalam waliobobea na muda mchache baada ya kupewa mtoto na ameongeza kuwa haijabainika kilichopelekea kifo chake na uchunguzi umeanzishwa.
Arwasa alisema kwamba hakukuwepo na utepetevu wa madaktari unaodaiwa kupelekea kifo Cha mama huyo.
Mwanamke huyo alijifungua mtoto msichana mwenye kilo 4.3 .