jimbo lapata sinodi ya kwanza

Jimbo katoliki la Eldoret limepata sinodi ya kwanza itakayodumu kwa mwongi moja.

Akiongea katika kanisa la Moyo mtakatifu wa Yesu Kathedrali,Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich akizindua sinodi hiyo amesema kuwa sinodi hiyo inalenga kurahisisha kazi ya kichungaji kwa kuwa Kila kaunti chini ya jimbo katoliki la Eldoret itasimamiwa na padre mkuu ambaye pamoja na askofu na padre mkuu wa jimbo watabuni kamati kuu ya jimbo.

Askofu kadhalika alisema kuwa sinodi hii itabuni kitengo ambacho kitakuwa kinashughulikia maswala ya familia na kingine cha kusikiza na kushauri mapadre na watawa katika jimbo katoliki la Eldoret na kutatua changamoto wanazopitia na kuwasaidia wanafamilia kuisha pamoja kwa upendo bila ya kuwa na chuki baina yao.

Askofu vilevile alisema kwamba kutakuwa na maswala mawili kuu ya kipastroli na yale yanayohusiana na ujenzi wa kanisa kupitia miradi mbalimbali na jinsi mkristu anavyostahili kujihusisha nayo.

Ikumbukwe kuwa utekelezwaji wa sinodi hiyo ikitarajiwa kuanza baada ya mwezi moja ili kuipa nafasi wakristu wote kudurusu na kuelewa yaliyomo kwenye sinodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *