Askofu Oginde; Kanisa la CITAM, Kusitisha Ibada Kanisani mwao

Kanisa la CITAM limestisha ibada zote za jumapili na zile za katikati ya juma katika harakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Katika kikao na wanahabari askofu mkuu wa kanisa hilo david oginde amesema ibada na shughuli zote katika kanisa hilo zitasitishwa kwa muda wa majuma matatu japo watakuwa wakipeperushwa mahubiri yao kupitia kwenye mitandao na hatas kwenye runinga.

Wahubiri wao wataongoza hafla za harusi na mazishi kwa kuzingatia maagizo yatakapotolewa japo kwa kuwataka wale wanajipanga kuwaanda harusi kuzihairisha kwa muda.

 Hata hivyo amewataka wakenya kushiriki katika kuliombea taifa hili siku ya jumamosi siku ambayo raisi uhuru Kenyatta ametangaza kuwa siku ya maombi ya kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *