Mafungo ya Kiroho: Mapambano ya kiroho katika sala na huduma!

Viongozi wa Kanisa wanapaswa kujizatiti katika mchakato wa kuwatafuta wale waliopotea; kujenga utamaduni wa kusahihishana na kuonyana kidugu; kusamehe, kusahau na kusali pamoja, ili kumwilisha huruma na upendo wa Mungu katika maisha yao.

Viongozi wa Kanisa waendelee kusimama kidete kulinda na kutetea utu, heshima na haki msingi za watoto, maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Wakeshe na kusali kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa; wawe tayari kusamehe na kusahau, tayari kuandika ukurasa mpya wa maisha na utume wa Kanisa. Kimsingi, huruma ya Mungu haina mipaka. Mtakatifu Petro, Mtume ni shuhuda makini wa huruma na upendo wa Mungu katika maisha yake! Alimkana Kristo Yesu mara tatu, akatubu na kujuta sana, kielelezo cha wale wote wanaotubu na kumwongokea Mungu kwani wanabarikiwa na kuwa ni vyombo na mashuhuda wa huruma na upendo wa Mungu!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *