Jumamosi tarehe 30 Mei mwaka huu saa kumi na moja unusu jioni majira ya Ulaya itaonyeshwa sala ya Rosari mubashara kutoka Grotto ya Lourdes katika bustani ya Vaticani,ambapo sauti ya Papa itainua maombi yake kwa Mama Bikira Maria kwa ajili ya kuomba msaada dhidi ya janga hili.Madhabahu yote ulimwenguni yanaalikwa kushiriki tukio hilo.
Mpango huo umeandaliwa na Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya na ambao utaona ujumuishwaji wa familia na wawakilishi wa kike na kiume wa sekta mbali mbali zinazohusika zaidi na kwa namna ya pekee walioathirika na janga hili, ambao watakabidhiwa kuongoza matendo ya Rosari.
Kwa njia hiyo ni pamoja na madaktari na wauguzi, wagonjwa waliopona na wagonjwa walioteseka katika kuomboleza kwa ajili ya ndugu zao, mkuu wa hospitali na mtawa mmoja muuguzi, mfamasia na mwandishi wa habari, na mwishowe mmoja wa kujitolea kutoka katika kikosi cha Ulinzi na usalama wa Jamii na familia yake, pia familia moja ambayo ilishuhudia kuzaliwa mtoto hasa katika wakati mgumu zaidi, ili kuelezea tumaini kwamba sio hakuna ulazima wa kushindwa na kukata tamaa.