Chifu waagizwa kusambaza Barakoa

Mbunge wa Keiyo Kusini Daniel Rono amewataka machifu wa eneo hilo kuhakikisha kuwa wakazi wanasambaziwa barakoa ili kuzuia maambukizi vya virusi vya korona kwa njia inayofaa.  

Akiongea katika kituo cha kibiashara cha Kamwosor wakati wa kupeana barakoa hizo kwa wafanyibiashara na wahudumu wa bodaboda, Rono alisema hatua hiyo itawasaidia wakazi kujikinga na ugonjwa huo wa covid 19.

Aidha mbunge huyo ametoa wito kwa maafisa hao wa utawala kuendeleza uhamasisho kuhusiana na virusi vya Corona kwa wenyeji hasa wale kutoka sehemu za mashinani ili wapate ufahamu wa yale wanafaa kuyazingatia.

Wakati uo huo Rono amewataka wakazi wa eneo hilo kuendelea kuzingatia maagizo yaliyotolewa na serikali kama njia moja ya kukabiliana na virusi hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *