Wito watolewa kwa rais na naibu wake kufanya mazungumzo

Baraza la wazee wa bonde la Ufa limetoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kufanya mazungumzo   ya kuleta udhabiti ndani ya chama cha Jubilee na kuupa umoja wa kitaifa kipaumbele.

Chinini na msimamizi Gilbert Kibage, baraza hilo limewashauri wawili hao kumaliza uhasama baina yao na kuangazia changamoto zinazoikumba taifa hili likiwemo janga la korona.

Wazee hao wanasema hali ngumu ya kiuchumi nchini inaweza kusababisha mgogoro ambao unaweza kuweka Kenya katika hali mbaya hata zaidi.

Wamesema licha ya wao kuunga mkono hatua ya rais Kenyatta kufanya kazi na vyama tofauti vya kisiasa, hali hiyo haifai kutumiwa kuwagawanya waenya kwa misingi ya vyama na kikabila.

Haya yanajiri huku chama cha Jubilee kikiwa kinalenga wandani wa Ruto kwenye kamati mbalimbali za bunge kwa kukikuka mwongozo wa chama, suala ambalo limeibua hisia kinzani kutoka pande husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *