Wito umetolewa kwa serikali kukubali hafla za ibada kuruhusiwa kuendelea katika viwanja vya makanisa badala ya ndani ya majengo hayo.
Hio ni kauli yake askofu wa makanisa ya Kianglikana humu nchini askofu Jackson Ole Sapit ikiwa na baada ya hatua ya muda sasa tangu kupigwa marufuku kwa makanisa nchini kwa lengo la kudhibiti virusi vya corona.
Askofu Sapitameyasema hayo akiwa kwenye kaunti ya Narok akisema kuwa kuandaliwa kwa hafla hizo nje ya kanisa itakuwa njia rahisi kutekeleza maagizo yanayotolewa na wizara ya afya hasaa ya kukaa umbali wa mita moja kutoka kwa mwingine na hivyo kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
Vilevile Sapit amesema kuwa wao kama kanisa wanaunga kikamilifu masharti ya serikali na hawangetaka kuwa kikwazo kwa jambo lolote.
Haya yanatukia wakti viongozi wa kidini mbalimbali wanazidi kutoa wito kwa serikali kuruhusu hafla hizo za ibada kuendelea kwani watatilia mkazo maagizo yoyote.