Usalama wadorora eneo la Huruma, Kaunti ya Uasingishu

Wakaazi wa mtaa wa Huruma mjini Eldoret wamelalamikia kudorora kwa usalama eneo hilo.

Haya yanajiri baada ya wezi kuvunja na kuingia katika nyumba 30 na kuiba vifaa vya kielektroniki.

Kwa mujibu wa mwakilishi wadi wa eneo hilo Peter Chomba, majambazi hao wanawabaka kina mama na kuwakatakata kwa upanga wakaazi  majira ya usiku licha ya kuwepo doria za polisi. Sasa wanaitaka serikali kutekeleza ahadi ya kuwajengea kituo cha polisi mtaani humo sawa na kuwataka wazee wa mitaa kuaandamana na polisi majira ya usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *