Jamaa mmoja eneo la Kipkeringon kaunti ya Nandi, amewaacha vinywa wazi wakaazi baada ya kumuua afisa wa NIS na mmliki wa nyumba aliokodi.
Inadaiwa kwamba mwanaume huyo alimtembelea mkewe katika soko ya Kipkeringon ambapo anaendesha biashara na kuanza kumshambulia. Wanandoa hao walianza kugombana na kumfanya mmilikiwa nyumba na afisa wa NIS kuingilia kati ili kutuliza hali.
Akiwa mwenye hamaki jamaa huyo alianza kuwashambulia watu waliofika eneo la tukio kujaribu kuwatenganisha ili wasiendelee kupigana na mkewe. Kulingana na mashahidi mwanaume huyo alianza kuwashambulia waliokuja kutuliza vurugu huku akiwadunga kisu watu watano.
Mmiliki wa nyumba hizo Edwin Cheruiyot Kogo, na Benjamin Sugut afisa wa NIS jijini Kisumu walifariki dunia wakipokea huduma za dharura katika hospitali ya Mosoriot.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa polisi, mshukiwa ambaye alitambulika kama Elkana Kiplimo Sitini alipelekwa katika hospitali ya Kabiyet ambapo anafanyiwa ukaguzi wa kiafya kubaini iwapo yuko na akili timamu. Aidha, majeruhi watatu walipelekwa katika hospitali ya Mosoriot kwa matibabu kisha wakagiizwa kurudi nyumbani baada ya hali yao kuimarika.