Taifa la Kenya hii leo limesajili visa vipya 25 vya watu walio na virusi vya corona na kufikisha 490 watu walioambukizwa ugonjwa huo .
Watu wengine sita wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani .katibu wa utawala katika wizara ya afya Mercy Mwangangi, amesema 15 kati ya visa hivyo ni kutoka Nairobi ilhali 10 ni kutoka Mombasa.
Kati ya visa hivyo vipya, 8 ni kutoka Eastleigh, 2 kutoka Kawangware, na 2 kutoka Umoja. Jumla ya sampuli 1,012 zimepimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Kisa cha umri wa chini sana ni cha mtoto mwenye umri wa miezi sita ilhali mwenye umri wa juu sana ni umri wa miaka 60. 13 kati yao ni wanaume ilhali 12 ni wanawake .
Mwangangi ametoa tahadhari kwamba hali ya kawaida haijarejelewa na kuonya kwamba wakenya hawafai kuendelea na shughuli za kawaida kana kwamba ugonjwa huo umethibitiwa.