Wahudumu wa afya watoa makataa ya wiki mbili kwa serikali

Siku chache tu baada ya kutimuliwa na maafisa wa polisi wakijianda kufanya maandamano yao, Sasa katibu mkuu wa wahudumu wa afya Seth Panyako amesema kama wafanyakazi wa afya wameipa serikali muda wa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanapokea marupurupu yao kufikia Mei 18.

Panyako amedai kuwa wafanyakazi hao hawajapokea malipo hayo licha ya wao kuwa mstari wa mbele dhidi ya kupigana na virusi hatari vya Corona.

Amesema kuwa wamekuwepo na mabishano baina ya serikali na viongozi wa wahudumu wa afya nchini kwa kile viongozi hao wanadai ni kunyanyaswa na kupendelewa kwa madaktari na serikali huku wahudumu wa afya wakiendelea kutaabika.

Viongozi hao sasa wanaitaka serikali kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa afya wanapewa vifaa muhimu vya kuwakinga dhidi ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *