Namna Virusi Vya Corona imetufanya Kugundua zaidi maana ya Kwaresma

Kwaresima ni kipindi cha mapambano ya “Jangwa la maisha ya kiroho” kwa kusikiliza, kutafakari na kumwilisha Neno la Mungu katika maisha.

Kwa kufunga na kusali; kwa njia ya matendo ya huruma: kiroho na kimwili, sanjari na kujikita katika maisha ya kisakramenti ili kupata: neema na baraka, toba na wongofu wa ndani. Kwaresima ni muda uliokubalika kwa waamini kujizatiti katika maisha ya kiroho kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Fumbo la Pasaka, yaani: Mateso, Kifo na Ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu!

Kwa njia hii, waamini wanakuwa kweli ni mashuhuda na vyombo vya Kristo Mfufuka kwa watu wa Mataifa! Huu ni mwaliko wa kujibu wito huu kwa uhuru mkamilifu unaochota nguvu zake katika Fumbo la Pasaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *