Wanafunzi kuanza masomo kupitia njia mbadala na shuleni

Wanafunzi kote nchini kuanzia wiki ijayo wataanza kupata masomo kupitia  Televisheni, redioni na ving’amuzi vingine vya  digitali.

Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa Elimu Prof George Magoha.

Haya yanajiri baada ya shule kufungwa  ghafla kufwatia mkurupuko wa virusi vya Corona nchini ambapo Rais Kenyattta aliagizi kuwa shule zote nchini Zikiwemo vyuo vikuuu na taasisi za kiufundi kufungwa ili kuepusha wanafunzi kuambukizana virusi.

Waziri alisema kuwa wizara imeshirikiana na televisheni ya kitaifa ya humu nchini kuwezesha vipindi vya masomo hayo kuanzia jumatatu kwa lugha zote mbili za kitaifa.

Magoha vile vile amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanawaangalia watoto wao haswa wakati huu ambao taifa limeripoti visa vingine vitatu vya virusi vya Corona na kufikisha idadi kuwa 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *