Mwanamume mmoja kwenye Kijiji cha Kubundani katika
Kaunti ya Kwale ameuliwa baada ya kutuhumiwa kwamba ameathirika na Virusi
vya Korona, kisa ambacho kimetokea usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na taarifa iliyonakiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Diani, George
Kotini Hezron ambaye alikuwa mlevi aliuliwa kilomita tatu kutoka eneo moja la
burudani.
Ripoti hiyo imebainisha kwamba kotini alikutana na kundi la vijana lililoanza
kumtuhumu kwamba anaugua ugonjwa wa Covid-19 baada ya ugomvi kuzuka baina
yake na kundi hilo.
Baadaye, vijana hao walimshambulia kwa mawe na kumjeruhi vibaya na
kufariki muda mfupi baadaye alipofikishwa katika Hospitali ya Msambweni.
Kamanda wa Polisi wa
Kwale Joseph Nthenge amesema msako dhidi ya waliotekeleza unyama huo
unaendelezwa.