Dalili za maambukizi ya virusi vya corona na mafua yanafanana kwa kiasi kikubwa, hivyo inafanya tiba kuwa ngumu bila kupimwa .
Dalili za virusi vya corona vinaweza kuanza kwa homa na kukohoa.
Mafua mara nyingi huwa yana dalili nyingine kama koo kuwasha, huku watu wenye virusi vya corona huwa wanaweza kuishiwa pumzi kidogo.
Ni mapema mno kuweza kulinganisha lakini virusi vyote vinaambukizwa.
Kwa wastani virusi vya corona vinaweza kuambukiza watu wawili au watatu huku virusi vya mafua huwa ni kama vinatoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine.
Ingawa maambukizi yote ya mafua na corona huwa yanasambaa kwa haraka.
Mtu mwenye maambukizi ya corona kama amepika bila kuzingatia usafi basi moja kwa moja anaweza kumuambukiza mtu mwingine virusi vya corona.
Virusi vya corona vinaweza kusambaa kwa matone ya kikohozi yaliyo kwenye mkono.
Kuosha mikono kabla ya kushika na kula chakula ndio ushauri unaotakiwa kuuzingatiwa.