Muungano wa Makanisa Wajadili BBI

Muungano wa makanisa umeandaa kongamano katika jumba la mikutano ya jumuia kwenye kaunti ya Kiambu, ili kupokea mafunzo kuhusiana na ripoti ya BBI kutoka kwa wataalamu wa sheria.

Baadhi ya viongozi wa kanisa hata hivyo wameelezea hofu yao kuhusiana na ripoti hio iliozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta huko Bomas, wakisema kuwa wanasiasa wamekuwa wakiitumia kuwagawanya wakenya hata zaidi. Baadhi yao hata hivyo wanahoji uhusiano na utumizi wa nyimbo za aina ya mtindo wa reggae, zinazotumika katika mikutano ya BBI na ripoti hio. Katika maoni yao kwenye kongamano hilo wametaka kujumuishwa kila mmoja katika mchakato huo wa kuwaleta wakenya pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *