Wakristu wameshauriwa siku zote kudhihirisha ukristu wao kwa kuwarekebisha wanaoteleza kwa upendo pasi na kuwabagua wengine na kuwakejeli wanapofanya kosa.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria alisisitiza haja ya kila mmoja anayesafiri kuelekea maisha ya kuurithi ufalme wa mbingu, kuwa na upendo na moyo wa kuwapatanisha wanaofarakana, kwa kuwa upendo huo unaweza ukaunganisha maadui na kuwaleta pamoja wakristu na jamii kwa ujumla wake.
Kauli ambayo imeungwa mkono na askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Nyeri Peter Kairo ambaye alisisitiza haja ya kila mkristu kutambuliwa kwa matendo mema na kuwa wenye kueneza upendo huo.