Viongozi waliochaguliwa nchini wameshauriwa kuwajibikia utendakazi wao na kusaidia kukomesha kero la ufisadi na maswala mengine ambayo yanarudisha nyuma shughuli za maendeleo nchini.
Kwa mujibu wa askofu wa jimbo katoliki la Embu Peter Kimani,viongozi wengi nchini hawana maadili yanayostahili kuigwa kwa kiongozi wa taifa na wanapaswa kubadili hilo kwa manufaa ya wananchi kupata maendeleo yaliyo bora.
Alisisitiza haja ya viongozi hao kuweka kando matakwa yao na kuangazia kikamilifu yale yanayowaongoza wananchi kwa hili wananchi wanaweza wakaheshimu na kuwa na imani nao.
Askofu Kimani aliwataka viongozi hao kumuiga aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye hadi kifo chake alikuwa kiongozi aliyeweka rohoni mwake maslahi ya wakenya na kuhakikisha kuwa hakuna yule ambaye angedhulumiwa.
