Askofu Kimengich:Kupiga kura ni haki yako

Wakenya wametakiwa kujitokeza na kujiandikisha kama wapiga kura haswa wakati huu ambapo tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inatekeleza zoezi hilo.

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich alisema kuwa ni haki ya kila mmoja  kidemokrasia kupiga kura na kuwachagua viongozi waadilifu, akitoa wito kwa vijana haswa wale wanoshabikia mageuzi nchini kutumia fursa hiyo kijiandikisha kama wapiga kura.

Alitoa wito kwa makamishna waliotwikwa jukumu la kuongoza tume hiyo kuweka mikakati ya kurejesha imani ya wakenya kwa tume hiyo, kwa kuhakikisha kuwa wanaandaa uchaguzi wa huru na haki, kwa kuwa ilivyo kwa sasa ni kuwa wakenya wengi walipoteza imani kwa tume hiyo, baada ya kuonekana kuandaa chaguzi zilizo na dosari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *