karata ya wawili yazalisha mauti Eldoret

mahakama kuu ya Eldoret iliwafunga siku ya jumanne maafisa wawili wa polisi kifungo cha miaka 35 gerezani kila mmoja baada yao kupatikana na hatia ya mauaji
 Jaji wa mahakama kuu ya Eldoret Reuben Nyakundi ambaye alitoa hukumu hiyo dhidi ya maafisa hao wawili Emmanuel wafula mwenye umri wa miaka 38 na Godwine sirengo mwenye umri wa miaka 35 amesema kwamba ushahidi ambao uliwasilishwa mahakamani kutoka kwa mashahidi 21 ulidhibitisha kwamba wawili hao walihusika na mauwaji ya Denis Lusava.

Nyakundi alisema kwamba kifo cha marehemu kingeepukika lakini maafisa hao wa polisi ambao wana jukumu la kulinda maisha walipelekea kupotea kwa maisha ya Lusava.

Kulingana na hati ya mahakamani wawili hao walitekeleza kitendo hicho mnamo mwaka wa 2020 ambapo iliarifiwa kwamba walimkamata lusava na.kumzuilia katika kituo cha polisi cha mbururu katika kaunti ya kakamega ambapo alipigwa na kuteswa kabla ya maiti yake kupatikana katika mto Nzoia siku chache baadaye.
Familia ya mwendazake ikiongozwa na Agnes Ambale ambaye ni mamake marehemu imesema kwamba imefurahia uamuzi wa mahakama wakisema haki,ikionekana kutendeka huku wakitaka maafisa wa polisi kupata funzo ili wasitende kitendo kama hicho kwa wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *