TUACHENI VITA

Baba Mtakatifu Leo XIV ametuma rambi rambi huko Congo,DR kufuatia shambulio ambalo watu zaidi ya arobaini walipoteza maisha yao.

Papa Leo kupitia ujumbe wake kwa njia ya Telegramu iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Vatican,Kardinali Parolin,Julai 28,Papa Leo XIV ametoa rambirambi kufuatia na shambulio la kigaidi la Julai 27,dhidi ya Kanisa la Mwenyeheri amu ya mashahidi iwe mbegu ya amani Anuarite katika kijiji cha Komanda,huko Congo DR ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya arobaini mikononi mwa washambulizi wa ADF.

Tukio lililotokea usiku wa kuamkia Dominika tarehe 27 Julai 2025 na kusababisha zaidi ya vifo arobaini. Katika Ujumbe huo ulielekezwa kwa Askofu Mkuu wa Lubumbashi, Fulgence Muteba Mugalu, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini DRC(CENCO) kwamba, Baba Mtakatifu Leo XIV amepata taarifa la shambulizi hilo kwa masikitiko makubwa ya kina katika Mkoa wa Ituri ambayo yalisabisha vifo vya waamini mikononi mwa magaidi wa ADF.

Papa Leo kwa njia hiyo anaungana na familia na jumuiya ya kikristo iliyoguswa huku akionesha ukaribu wake na kuwahakikishia maombi yake.
baba Mtakatifu vilevile anasema anamuomba Mungu ili damu ya mashahidi hawo iweze kuwa mbegu ya kupanda amani, maridhiano , udugu na upendo kwa watu wote wa Congo.

Katika muktadha huo anatuma baraka yake ya kitume kwa Parokia ya Mwenyeheri Anuarite wa Komando, kwa namna ya pekee familia nyingi zilizoguswa na msiba huo kwa wana na binti wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC na Taifa zima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *