Mbolea sasa iko tayari NCPB

Serikali imesema imejitolea kuhakikisha kwamba uzalishaji wa chakula nchini inaongezeka kupitia kwa kuweka sera za kudumu.

katibu katika wizara ya kilimo Paul Rono akizungumza alipozuru maghala ya nafaka na mazao ya NCPB jijini Eldoret, amewahakikishia wakulima kwamba serikali itaendelea kutoa pembejeo kwa wakati ufaao ili kuongeza kapu la chakula nchini.

kwa upande wake,meneja wa NCPB ukanda wa North Rift Gilbert Rotich amewataka wakulima kujitokeza ili kupokea mbolea yao akisema kila mkulima aliyejisajili atapokea kiwango hitajika.

Wakati huo,afisa msimamizi wa kampuni ya kusambaza mbegu nchini Sammy Chepsisor amesisitiza kwamba mbegu inapatikana kwa bei iyowekwa na serikali na hakuna haja wakulima kuhofu kuwa watakosa bidhaa hiyo.

yanajiri haya wakati na ambapo,wakulima wakulima siku za hivi karibuni walikuwa wamejitokeza na kulalamikia ukosefu wa mbolea na mbegu swala lililoibua mihemko miongoni mwa washikadau wa sekta ya kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *