Serikali kupitia asasi zote husika imetakiwa kuweka mikakati maalum ili kuleta mageuzi nchini na kutekeleza ahadi iliyoahidi wakenya kuelekea uchaguzi mkuu ulipita.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa Martin Kivuva Musonde amesema kuwa hatua ya kubuniwa kwa tume huru na mipaka nchini IEBC ni hatua muhimu ambayo itahakikisha wakenya wanapata haki ya kidemokrasia ikizingatiwa kuwa kuna maeneo ambayo kwa sasa yanahitaji uwakilishi kutokana na kufariki kwa wawakilishi wao na wengine kuteuliwa kushikilia nyadhifa mbalimbali katika serikali kuu.
Mojawapo ya maeneo hayo ni kaunti ya Uasin gishu katika wadi ya Tembelio aqmbapo mwakilishi wadi Evans Kapkea alichaguliwa kuwa naibu gavana wa kaunti ya Uasi ngishu baada ya Mhandisi John Barorot kujiuzulu wadhifa huo.
Hata hivyo askofu mkuu kivuva ametaka serikali kuweka bidi ya kushughulikia maswala ya eliimu nchini na afya ambayo anasema kuwa kwa sasa inakumbwa na changamoto si haba.
Kadhalika ametoa wito kwa asasi za kiusalama kuhakikisha kuwa wakenya wote wanasalia huru akitaka kukomeshwa kwa visa vya mauaji na utekaji nyara mabayo vinashuhudiwa nchini.