Familia yapapasa ufisadi

Familia zimetakiwa kujikita katika swala la uadilifu kama njia moja ya kuweka msingi dhabiti wa kupambana na ufisadi nchini.

Mwenyekiti wa kamati ya haki na Amani kwenye baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB ambaye pia ni askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Simon Peter Kamomoe amezitaka familia kuweka matumaini yao katika kukuza uadilifu kwa kuwa chanzo cha ufisadi ni kutoka katika familia.

Askofu Kamomoe amesema kuwa matatizo ambayo wakenya kwa sasa wanapitia ni kutokana na kukubali kuhongwa na wanasiasa kuelekea uchaguzi mkuu uliopita akitoa wito kwa kila mkenya kutekeleza haki yao ya kidemokrasia bila kupokea hongo.

Askofu kadhalika amesema kuwa kina mama kuwahudumia mapadre na maaskofu kushinda waume wao kadhalika ni ufisadi ambayo inastahili kukomeshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *