Askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima ametoa wito kwa kila mkristu kutumia kipindi cha kwaresima kujenga upya uhusiano kati yao na mwenyezi Mungu kwa kutubu na kutenda matendo ya kiutu.
Akihubiri katika misa ya uzinduzi wa kampeni ya kipindi cha Kwaresima askofu Kadima amesema kuwa toba na matendo ya kiutu siku zote ni kwa utukufu wa mwenyezi Mungu na wala sio shuruti ya kanisa kama vile wengi wanavyodhani
Ametoa wito kwa kila mmoja kumtegemea kristu katika kila hali wanayopitia kwa sasa akisema kuwa kristu ndiye mpaji wa kila kitu katika dunia hii ambayo imejaa kelele nyingi.
Amewataka wakatoliki wasadiki kuwa wao ni watenda dhambi na neema ambayo hupyaisha maisha yao na kujenga uhusiano kati yao na mwenyezi Mungu ni kupitia toba.