Kenya bila upinzani itazama

Askofu wa jimbo katoliki la Lodwar John Mbinda ametoa wito kwa serikali kushughulikia maslahi ya wakenya na kuwatekelezea ahadi ilizotoa kuelekea uchaguzi mkuu uliopita.

Askofu Mbinda amekosoa hatua ya upinzani kuungana na serikali na baadhi ya viongozi kujumuishwa kwa serikali akisema kuwa taifa la kenya huenda likajipata pabaya kwa kuwa asasi za serikali zitafeli kuwajibishwa na upinzani.

Kadhalika askofu huyo amekariri kuwa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki litaendelea na kukosoa serikali inapoteleza na kutoa mwelekeo ambayo serikali inastahili kufuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *