KCCB kuandaa maombi ya kitaifa oktoba tatu

Maandalizi ya siku ya kitaifa ya maombi yanayoongozwa na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki yameshika kasi huku maadhimisho hayo yakiratibiwa kufanyika tarehe tatu mwezi October mwaka huu.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika eneo la Sala la Subukia Jimbo katoliki la Nakuru ambapo Jimbo kuu katoliki la Kisumu likitarajiwa kuongoza liturjia ya mwaka huu.

Hata hivyo kamati andalizj ya maadhimisho haya ya maombi ya kitaifa imekadiria kupokea mahujaji elfu thelathini kutoka katika Jimbo kuu katoliki la Kisumu kamati hiyo kadhalika ikitoa wito wa hija kutoka kwa mahujaji wa majimbo mengine.

Naibu mwenyekiti wa walei kwenye Baraza la maaskofu askofu Wallace Nganga ametoa wito kwa wakristu kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo Akitoa wito kwao kuangazia kwa kina unyenyekevu, uvumilivu na umakinifu katika sala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *